Mnamo
tarehe 18.05.2016 majira ya saa 20:30hrs katika msikiti wa masjid
rahman uliopo ibanda relini mtaa wa utemini @ mapankini kata ya mkolani
wilaya ya nyamagana jiji na mkoa wa mwanza.
Watu
wasiozidi 15 wakiwa wamevalia mavazi ya kuficha uso wakiwa na mapanga,
shoka na bendera nyeusi yenye maandishi meupe waliingia ghafla katika
msikiti tajwa hapo juu wakati waumini wa msikiti huo wakiwa wanaswali na
kuzima taa na kutoa sauti wakisema “kwa nini mnaswali wakati wenzetu
wamekamatwa na wanashikiliwa na polisi ?” na hapo hapo wakaanza kuwakata
kwa mapanga baadhi ya waumini katika sehemu mbalimbali za miili yao.
Walipata
majeraha makubwa kichwani, shingoni na mikononi na walipoteza maisha
yao papo hapo na mmoja kupata majeraha sehemu za kichwani na kukimbizwa
hospitali ya wilaya ya nyamagana (butimba).
Waliouawa,
1. Feruz ismail elias mika 27, muha imamu wa msikiti huo na mkazi wa
ibanda relini, 2. Mbwana rajab miaka 40, mbondei mfanyabiashara na mkazi
wa ibanda, 3. Khamisi mponda miaka 28 dereva wa kiwanda cha samaki
(TFP), mkazi wa mkolani, wote walijeruhiwa sehemu za kichwani, shingoni
na mikononi.
Aliyejeruhiwa
ni ismail abeid @ ghati miaka 13, mkurya mwanafunzi wa madrasa katika
shule ya kiislamu itwayo jabar hila iliyoko maeneo ya Nyasaka aliyepata
majeraha kichwani na anapata matibabu hospitali ya Nyamagana.
Kutokana
na hali hiyo, waumini wengine walifanikiwa kukimbia huku wakipiga
mayowe yaliyopelekea wahalifu hao kukimbia na kurusha ndani ya msikiti
chupa mbili za konyagi zilizokuwa na petroli na tambi za moto, chupa
moja ililipuka lakini haikuleta madhara makubwa.
Jeshila
la polisi limewakamata washukiwa watatu kwa ajili ya kuwahoji
kuhusiana na tukio hilo, huku msako mkali wa kuwasaka watu wengine walio
husika kwa namna moja au nyingine kwenye mauaji hayo ukiwa bado
unaendelea.
Napenda
kuwaeleza wananchi watulie wakati tukiendelea na upelelezi wa tukio
hili, na natoa wito kwa wananchi kushirikiana na jeshi la polisi kwa
kutoa taarifa za wahalifu wa mauaji hayo ili tuweze kuwakamata.
Pia
nashauri na kusisitiza kuwepo na kamati za ulinzi na usalama katika
nyumba za ibada, kumbi za starehe pamoja na mitaa yao. Hii itasaidia kwa
kiasi kikubwa kuimarisha ulinzi na usalama katika maeneo hayo.
Imesainiwa na:
……………………….
Sacp: Ahmed Msangi
Kamanda wa Polisi (m) Mwanza.
Post a Comment