Makubaliano ya
kusitisha mapigano nchini Syria yamepata pigo kubwa baada ya waasi ambao
ni washirika wa wanamgambo wa al-Qaeda nchini Syria kudungua ndege ya
jeshi la Syria iliyokuwa ikipeleleza maficho ya waasi karibu na mji wa
Aleppo.
Hili ni tukio la pili baada ya ndege nyingine ya kijeshi kudunguliwa mwezi Machi.
Waasi hao wanaoungwa mkono na Marekani wamekuwa wakiomba msaada wa makombora yenye uwezo wa kudungua ndege ilikujikinga dhidi ya mashambulizi ya angani yanayotekelezwa na jeshi la Syria na washirika wake wakiongozwa na Urusi.
Katika video hiyo rubani huyo anaonekana akitaja jina lake na sehemu anayotokea ambayo ni Latakia
Jeshi la Bashar al Assad limekiri kupoteza ndege hiyo na pia rubani wake aliyekwepa kwa mwavuli lakini kwa bahati mbaya akatekwa nyara.
Shirika la kupigania haki za kibinadamu Syrian Observatory for Human Rights limesema kuwa rubani huyo amefungiwa katika makao makuu ya Al Nusra Front.
Post a Comment