0


Visa vya kujua vimeongezeka miongoni mwa wanawake wa umri wa makamo 
 
Takwimu rasmi za serikali zinaonesha idadi ya watu wanaojiua nchini Marekani imepanda pakubwa.

Takwimu hizo kutoka kwa Kituo cha Taifa cha Takwimu za Afya zinaonyesha viwango vya watu kujiua vimeongezeka kwa karibu asilimia 25 katika kipindi cha miaka 15 iliyopita.

Visa vya watu kujiua vimefikia kiwango cha juu ambacho hakijawahi kushuhudiwa tangu miaka ya 1980.

Utafiti huo uliangazia watu wa jinsia zote na marika yote.

Viwango vya wanawake kujiua ndivyo vilivyoongezeka zaidi, vikipanda kwa asilimia 36 miongoni mwa wanawake wa umri wa makamo.

Visa vya wasichana wa umri wa kati ya miaka kumi na 14 vimeongezeka mara tatu katika kipindi hicho.

Wataalamu wanasema hili huenda limesababishwa na matumizi ya mitandao ya kijamii pamoja na watu kudhalilishwa mtandaoni.

Visa vya watu kujiua miongoni mwa Wamarekani asilia vilipanda zaidi, karibu asilimia 90, ingawa visa vya kujiua miongoni mwa wanaume weusi vilishuka kiasi.

Profesa Robert D Putnam kutoka Chuo Kikuu cha Harvard anasema ushahidi zaidi unapatikana ukionesha uhusiano baina ya umaskini, kutamauka na hali ya afya.

Post a Comment

 
Top