0
  Rashford amefunga mabao saba katika mechi 13 
 
Meneja wa timu ya taifa ya England Roy Hodgson amesema atakuwa na uamuzi mgumu wa kufanya kabla ya kumchukua mshambuliaji chipukizi wa Manchester United Marcus Rashford kwenye kikosi chake cha Euro 2016.

Rashford, 18, amefunga mabao saba katika mechi 13 tangu aanze kuchezea timu kubwa Februari.
Hodgson amependezwa sana naye lakini amesema itakiwa vigumu sana kwake kumuweka kwenye kikosi cha Ufaransa.

“Nafikiri utakuwa uamuzi jasiri sana kumuingiza kikosini,” ameongeza Hodgson.
Rashford, amesalia na miezi sita atimize umri wa miaka 19.

Alichezea timu kubwa ya Manchester dhidi ya FC Midtjylland katika Europa League na akawafungia mabao mawili.



Hodgson ana washambuliaji wengi sana anaoweza kutumia 
 
Hodgson ana washambuliaji wengi wakiwemo Wayne Rooney (Manchester United), Harry Kane (Tottenham), Jamie Vardy (Leicester City), Daniel Sturridge (Liverpool) na Danny Welbeck (Arsenal).

Kuna pia Andy Carroll wa West Ham.

"Inaonekana kwamba itakuwa vigumu (kumchukua) lakini ukizingatia wachezaji anaoshindana nao, itakuwa vigumu kiasi,” amesema Hodgson.

Post a Comment

 
Top