Unene wa kupindukia
umehusishwa na ongezeko la idadi ya wanawake wanaopatikana na saratani
ya kizazi. Hii ni kwa mujibu wa Taasisi ya utafiti wa Saratani
Uingereza.
Hata hivyo wamesema utafiti zaidi unahitajika. Nchini Uingereza wanawake 9,000 hugunduliwa na saratani ya kizazi kila mwaka huku 2000 wakifariki dunia kutokana na ugonjwa huo.
Watafiti wanasema matibabu yake yameimarika na kwamba wagonjwa wengi wanapona.Kwa mujibu wa Profesa Jonathan Lederman wa Taasisi ya Saratani Uingereza, siyo kwamba unene unasababisha saratani lakini unahatarisha kupata ugonjwa wenyewe.
Baadhi ya mambo mengine yanayoweza kuhatarisha kupata saratani ni pamoja na kutofanya mazoezi, umri, chakula na maumbile.
Post a Comment