Zaidi ya nusu ya
kura zilizohesabiwa katika uchaguzi wa awali wa urais nchini marekani
katika mji wa New york,zinaonesha kwamba Donald Trump na Hillary Clinton
wamepata ushindi mkubwa Zaidi ndani ya vyama vyote viwili.
Hata hivyo New York inatajwa kuwa ngome nyingine ya Donald Trump,ambapo Cruz yeye hesabu za kura zake zimeonekana kugoma mapema kabisa katika chama chake cha Repubilcan .
Wakati Hillary Clinton amemshinda mpinzani wake Bernie Sanders kwa ushindi mkubwa .Hillary amewaambia wapinzani wake kuwa kuna la ziada linalowafanya wawe wamoja Zaidi ya kuwagawa.
Post a Comment