Mwenyekiti wa TCCIA Mkoa wa Iringa, Lucas Mwakabungu aliyasema hayo jana kwenye warsha ya mafunzo ya Dawati la Majadiliano kati ya sekta ya umma na binafsi, iliyofanyika kwa siku mbili mjini hapa.
“Uamuzi huo wa rais wetu utasaidia sana kushusha riba za mabenki yetu ya biashara kwa sababu sekta binafsi ndiyo itakayokuwa mteja mkubwa wa mabenki hayo,” alisema Mwakabungu.
Pamoja na kuipongeza serikali kwa kazi kubwa inayofanya ya kuboresha mazingira yanayokuza sekta binafsi, Mwakabungu alisema bado mazingira ya biashara yameendelea kuwa katika changamoto nyingi.
Alizitaja baadhi ya changamoto hizo kuwa ni pamoja na kodi nyingi, masoko ya bidhaa na huduma kutokuwa ya uhakika, miundombinu mibovu ya barabara na ukosefu wa umeme vijijini, matumizi ya pembejeo bandia na sheria ya vipimo na mizani kutosimamiwa ipasavyo.
Nyingine zinahusu wakulima kuuza mazao yao kwa bei ya chini ya gharama za uzalishaji kwa sababu ya ukosefu wa bei elekezi, ukubwa wa ushuru wa mazao na ulipaji wa leseni za biashara ambao ni kikwazo kikubwa katika urasimishaji wa biashara.
Kwa kupitia warsha hiyo ambayo mbali na kushirikisha wawakilishi toka sekta binafsi, iliwashirikisha pia wakuu wa wilaya, wakurugenzi na wenyeviti wa halmashauri za mkoa wa Iringa, Mwakabungu alisema wadau hao wamepata stadi juu ya umuhimu wa majadiliano kati ya sekta binafsi na ya umma ili kuharakisha maendeleo.
Akifungua warsha hiyo, Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Amina Masenza, alisema ushirikiano kati ya sekta ya umma na binafsi ndio utakaoihakikishia maendeleo nchi.
“Naomba TCCIA kwa kushirikiana na waandaji wa warsha waangalie pia uwezekano wa kutoa mafunzo hayo ya meza ya pamoja kwa ngazi ya wakuu wa idara zote za halmashauri na madiwani wake ili wawe katika mkakati wa kuboresha mazingira hayo,” alisema.
Post a Comment