0


 
                               Wenyeji wa Congo Brazzavile wakitoroka makwao
Jeshi la Congo-Brazzaville limeshambulia kwa mabomu vijiji vilivyoko Kusini mwa Poole na kusababisha maafa makubwa

Shirika la kutetea haki za binadamu Amnesty International linasema kuwa jeshi la taifa lilishambulia vijiji kwa ndege za helikopta na kusababisha uharibifu mkubwa.

Makanisa shule na hata zahanati za afya katika eneo la Poole lililoko Kusini mwa Congo Brazzaville zililengwa.

Walioshuhudia wanasema kuwa helikopta za kijeshi zilishambulia vijiji vya Vindza kwa zaidi ya mabomu 30.

Inadaiwa kuwa nyumba iliyolengwa ilikuwa makao ya Frederic Ntumi ambaye alikuwa akihudumu kama kiongozi wa kidini kijijini humo.
 
Nyumba iliyolengwa ilikuwa ya Pastor Ntumi anayedaiwa kuongozi kundi la waasi wa Ninja
Kasisi huyo anadaiwa kuongoza kundi la waasi la Ninja.

Mashambulizi hayo yanadaiwa kutekelezwa na jeshi Aprili tarehe 5 siku moja tu baada ya mashambulizi kutokea katika mji mkuu Brazzaville.

Waasi hao wanadaiwa kushambulia kambi ya kijeshi pamoja na vituo vinne vya polisi.
 
Walioshuhudia wanasema kuwa helikopta za kijeshi zilishambulia vijiji vya Vindza kwa zaidi ya mabomu 30.
Kundi la waasi la Ninja liliwahi kuwa na nguvu na wafuasi wengi katika miaka ya 1997-1999 lakini likavunjiliwa mbali kufuatia makubaliano ya amani yaliyotiwa sahihi mwaka wa 2003.

Wakati huo Ninja walikuwa ni wafuasi wa waziri mkuu wa zamani Bernard Kolelas ambaye ni babake mgombea wa urais Guy-Brice Parfait Kolelas, aliyejizolea asilimia 15 % ya kura katika uchaguzi wa urais uliofanyika mwezi Machi mwaka huu.

Post a Comment

 
Top