Kampuni ya Bia Tanzania (TBL)
Tuzo hiyo ilitolea katika shindano la kuonja vinywaji hicho
lililoandaliwa na kampuni ya SabMiller na kushirikisha wafanyakazi wake
wenye utaalam wa kuonja vinywaji kutoka katika viwanda vyake vilivyopo
sehemu mbalimbali duniani.
Aliyeibuka mshindi wa tuzo hiyo ni Rebecca Semoka, kutoka Kiwanda
cha Ilala jijini Dar es Salaam ambaye amekuwa muonjaji bora wa bia
kutoka barani Afrika katika shindano ambalo hufanyika kila mwaka chini
ya usimamizi wa kampuni ya kimataifa Aroxa inayoshughulika na usimamizi
wa ubora wa bidhaa zinazozalishwa viwandani.
Mwaka huu shindano hilo lilijumuisha washindani kutoka mabara ya
Afrika, Ulaya, Asia, Latin America na Amerika ya Kaskazini na hivyo
Rebecca kuibuka mshindi kutoka Bara la Afrika.
Akizungumzia ya ushindi huo, alisema kuwa unatokana na elimu yake,
mafunzo na mazoezi mbalimbali ambayo amekuwa akiyapata katika kampuni
anayofanyia kazi ya TBL Group.
Post a Comment