Kundi la Taliban nchini Afghanistan limetangaza kuanza kwa msimu wao wa mashambulizi.
Wanamgambo hao walisema kwenye taarifa kuwa, wataendesha mashambulizi makubwa kote nchini Afghanistan.Taliban wameyapa jina mashambulizi hayo kuwa "Operation Omari" kwa heshima ya mwaanzilishi Mullah Muhammad Omar ambaye kifo chake kilithibitishwa mwaka uliopita
Serikali ya Afghanistan inajaribu kulileta kundi hilo kwenye meza ya mazungumzo ili kumaliza mzozo kati yao.
Wakati ya ziara yake nchini Afghanistan, waziri wa mashauri ya nchi za kigeni nchini Marekani John Kerry, aliwataka Taliban kufanya mazungumzo ya moja kwa moja na serikali.
Post a Comment