Vyama vikuu vya
kisiasa nchini Ukrain vitajaribu kumteua waziri mkuu mpya baadaye hii
leo, huku kukiendelea kushuhudiwa msukosuko wa kisiasa.
Waandishi wa habari wanasema kuwa rais wa Ukrain Petro Poroshenko, yuko chini ya shinikizo kubwa kutoka kwa washirika wa nchi hiyo, wakiwemo muungano wa ulaya na marekani pamoja na watu nchi hiyo wanaotaka kuwepo mabadiliko kamili.
Maafisa saba wameondoka serikalini siku za hivi majuzi wakilalamika kuwa serikali haijajitolea kupambana na ufisadi.
Post a Comment