Joka kubwa zaidi kuwahi kukamatwa duniani amekufa.
Joka hilo linakisiwa kuwa takriban mita 8 hivi sawa na futi 26 lilipatikana siku ya Alhamisi iliyopita.
Afisa anayesimamia ujenzi katika kisiwa hicho cha Penang, Herme Herisyam aliiambia BBC.
Kulingana na daftari za kumbukumbu za Guinness, joka anayeshikilia rekodi ya dunia anaurefu wa mita 7.67.
Chatu huyo anayeitwa Medusa ana uzani wa kilo 158 na anaishi katika jumba moja mjini Kansas City, Missouri Marekani.
Hata hivyo joka huyo wa Malaysia ambaye alikuwa mkubwa zaidi yake hakuwa amepimwa na kuthibitishwa kuwa mrefu zaidi kabla ya kufa kwake.
Bw Herisyan anasema kuwa alikuwa na uzani wa kilo 250.
Hata hivyo katika harakati za kumuokoa kutoka maficho yake inakisiwa kuwa aliumia na hivyo akafa kabla hajafikishwa kwenye hifadhi ya wanyama alikotarajiwa kutuzwa hadi ajifungue.
Post a Comment