Wagombea waliobaki
kwenye kinyanganyiro cha kuwania urais nchini Marekani, wanang'ang'ania
kura muhimu zaidi za mchujo hii leo katika jimbo la New york. Likiwa
moja ya majimbo makubwa nchini Marekania lina ushawishi mkubwa kwa
wagombea wote.
Kwa upande wa Republican mgombea mkuu Donald Trump ni mwenyeji wa jimbo hilo.
Ananuia kupata ushindi dhidi ya mshindani wake mkuu Ted Cruz, Lakini amekosoa mbinu ya kumchagua mgombea wa chama.
Mshindani wake mkuu Ted Cruz hatarajiwi kufanya vyema baada ya kukosoa sera za Trump mapema kwenye kampeni.
Post a Comment