0


Makamu wa rais wa China kushoto na rais wa Korea Kaskazini King Jong Un
China imeiwekea vikwazo vya kibiashara Korea Kaskazini ikitangaza marufuku ya kuingiza dhahabu na mkaa pamoja na kuliuzia taifa hilo mafuta ya ndege sambamba na masharti ya Umoja wa Mataifa.
Wizara ya biashara pia imepiga marufuku uingizaji wa vyuma adimu duniani vinavyotumiwa katika bidhaa za kiufundi.

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa lilipiga kura mwezi Machi ya kuongeza vikwazo hivyo dhidi ya Korea Kaskazini.

Uamuzi huo wa pamoja unajiri baada ya Korea Kaskazini kufanya jaribio jingine la silaha zake za kinyuklia mnamo mwezi Januari na kuzindua kombora jingine la masafa marefu mwezi uliofuatia.
                                                    Korea Kaskazini
Mwandishi wa BBC huko Shanghai anasema kuwa hatua hiyo inakaribia uidhinishaji wa vikwazo vya Umoja wa Mataifa ambavyo China iliunga mkono.

Wengine wana wasiwasi kwamba Beijing haifuatilii vikwazo hivyo.

Post a Comment

 
Top