Mshukiwa wa shambulio la Paris aliyenusurika Salah Abdeslam alikataa kujilipua ili kuokoa maisha ,nduguye amesema.
Kungekuwa na waathiriwa zaidi iwapo ningefanya hivyo,Salah alimwambia nduguye.
Shambulio la ufyatuaji risasi pamoja na lile la bomu katika ukumbi mmoja wa tamasha,uwanjani,mgahawani na baa moja mnamo tarehe 13 mwezi Novemba liliwauwa watu 130 mnamo mwaka 2015.
Abdeslam mwenye umri wa miaka 26 alikamatwa mwezi uliopita mjini Brussels siku nne kabla ya shambulio la bomu mjini Brussels lililowaua watu 32.
Raia huyo wa Ufaransa aliyezaliwa mjini Ubelgiji alikuwa mafichoni katika mji huo mkuu wa Ubelgiji kwa zaidi ya miezi minne.
Baada ya kukamatwa Abdeslam alihojiwa kuhusu jukumu lake katika mashambulio hayo ya Paris.


Post a Comment