Rais wa Marekani Donald Trump ameadhimisha siku mia moja uongozini kwa kutoa hotuba ya kushambulia wanahabari na kutetea mafanikio yake.
Bwana Trump amewaaambia wafuasi wake huko Pennsylvania kwamba ameridhika kuwa pamoja nao badala ya kuhudhuria dhifa ya chakula cha jioni na wanahabari ama 'Correspondents diner' iliyokuwa ikifanyika katika ikulu ya White House wakati huo.
Hafla hiyo ni miongoni mwa hafla maarufu sana mjini Washington.
- Trump aionya tena Korea Kaskazini
- Trump: tutaidhibiti Korea Kaskazini
- China yataka Marekani na Korea Kaskazini kuvumiliana
Akihutubia umati mkubwa katika jimbo la Pennsylvania, Rais Trump amelinganisha na kutofautisha, kile ametaja 'siku mia moja za wanahabari kushindwa na kazi yao', na mafanikio yake ambapo amesema amekuwa akitimiza 'ahadi zake kila siku', hususan kurejesha kazi za viwanda na kumaliza mzozo katika sekta ya makaa ya mawe.
Pennsylvania ni jimbo linalotegemea uchumi wa uchimbaji madini, na lilikuwa muhimu sana katika uchaguzi wa mwaka jana.
Awali maelfu ya watu waliandamana nchini Marekani dhidi ya utawala wa rais Trump na msimamo wake kuhusu mazingira.
Post a Comment