Mbwana Samatta hakamatiki. Mchezaji huyo amezidi kuendeleza kasi yake ya ufungaji katika klabu ya KRC Genk.
Jumapili hii nahodha huyo wa Taifa Stars amefanikiwa kufunga goli
moja katika ushindi wa mabao 4-0 walioupata Genk wakiwa ugenini dhidi ya
KVC Westerlo.
Samatta alifunga goli lake katika dakika ya saba ya mchezo huo huku
magoli mengine yakifungwa na Thomas Buffel dakika ya 27, Omar Colley
dakika ya 67 na Ruslan Manilovskydakika ya 90.
Mpaka sasa Samatta amefanikiwa kufunga magoli matano ndani ya wiki
moja yakiwemo mawili aliyofunga Alhamisi iliyopita katika michuano ya
kombe la Europa League.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment