Kesi
ya Dawa za kulevya inayomkabili muigizaji wa filamu nchini Tanzania,
Wema Sepetu iliyokuwa isikilizwe leo, imeahirishwa hadi Aprili 11 mwaka
huu baada ya upande wa mashtaka kudai kuwa upelelezi haujakamilika.
Muigizaji
huyo ni mmoja kati ya wasanii ambao walitajwa kwenye list ya mkuu wa
mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda yawatuhumiwa wanaojihusisha na
biashara ya dawa za kulevya.
Post a Comment