Wabunge
Hussein Bashe wa Nzega Mjini na Joseph Kasheku wa Geita wakiwa na
aliyewahi kuwa mbunge wa Kisarawe, Adam Malima wamehojiwa polisi na
kisha kuachiwa baada ya kukamatwa kwa tuhuma za kupanga njama za
kuvuruga mkutano mkuu wa CCM
Inaelezwa
kuwa, wabunge hao ambao ni wajumbe wa mkutano mkuu maalum wa CCM, ambao
unatarajiwa kufanyika kesho, Machi 12 mjini Dodoma walikuwa wakipanga
njama za kuvuruga mkutano huo kwa kugawa pesa kwa baadhi ya wajumbe.
Kamanda
wa Polisi mkoani Dodoma amethibitisha kukamatwa kwa wabunge hao, kwa
ajili ya mahojiano, lakini amesema kuwa baada ya mahojiano, wabunge hao
wameachiwa kwa dhamana baada ya kujidhamini wao wenyewe.
"Walikuwa
wanahojiwa tu lakini kwa sasa wameshaachiwa, kulikuwa na tuhuma kwamba
wanagawa hela wanapanga kuvuruga mkutano wa CCM, wamejidhamini wenyewe,
na upelelezi bado unaendelea ili kubaini kama ni kweli" Amesema Kamanda
Mambosasa
Kuhusu
endapo watu hao walikutwa na pesa, Kamanda amesema mmoja kati yao
amekutwa na pesa lakini akadai kuwa ni pesa zake kwa ajili ya matumizi
binafsi.
Post a Comment