0



Sasa Wema Sepetu na Batuli ni mbuzi na chui, urafiki ndio umefika mwisho. Tukio hilo limetokea baada ya Wema kukasirishwa na kitendo cha Batuli kusema kuwa yeye alishalipwa fedha zake za kampeni na CCM.

Kupitia mtandao wa Instagram, Wema Sepetu ameweka picha ya rafiki yake huyo wa zamani na kuandika ujumbe ambao umeashiria kuwa urafiki wao ndio basi tena.


“Neno Moja Kwake…! Temporary Post… Mimi naanza… Alikuwa Rafiki yangu na Tulipendana sana….,” ameandika Wema kwenye picha ya Batuli hiyo hapo juu aliyoiweka kwenye mtandao huo.

Baada ya ujumbe huo wa Wema, Nay wa Mitego amemchochea muigizaji huyo ambaye wote kwa sasa wanakisupport Chadema kwa kuandika, “ @wemasepetu #MudaWetu Wana Maneno Mengi Tatizo Hawa Action… Usi mwamini ndugu Ata Rafiki, wachukulie Wote wanafiki, ishi tu kivyako Binadamu awa aminiki..!

Post a Comment

 
Top