0


Dar es Salaam. Wanamuziki Ally Kiba na Diamond Platnumz ni miongoni wa wajumbe wa kamati ya watu 10 wa kusaidia maandalizi ya timu ya taifa ya vijana ya Tanzania  'Serengeti Boys'

Akitangaza kamati hiyo inayoundwa na wanahabari, viongozi wa kampuni na wasanii Waziri wa Habari, Utamaduni Sana'a na Michezo Nape Nnauye amesema jukumu kubwa la kamati hiyo ni kuhakikisha wananchi wanashirikishwa kwenye maandalizi ya timu hiyo.

"Tumeshamiria kuona timu hii inafanya maandalizi makubwa na nimeongea na Malinzi asubuhi hii yuko Morocco akiweka sawa masuala ya kambi ya vijana,"amesema.

Kamati hiyo itakuwa chini ya uenyekiti wa mwanahabari mkongwe Charles Hillary na katibu ni katibu mkuu wa TFF, Mwesigwa Selestine.

Wajumbe wa kamati hiyo ni wanamuziki Ally Kiba na Diamond Platnumz wengine ni Beatrice Singano, Ruge Mutahaba, Maulid Kitenge, Erick Shigongo, Hassan Abbas na mwanamitindo Hoyce Temu.

Serengeti Boys imefuzu kucheza fainali za vijana Afrika nchini Gabon Mei 24- Juni 5, baada ya kushinda rufani yake dhidi ya Congo-Brazzaville iliyomchezesha mchezaji Langa Lesse Bercy ambaye umri wake ulizidi miaka 17.

Post a Comment

 
Top