0


Utawala binafsi ni vile mtu anaweza kuishi katika maagano na malengo yake kwa kuzingatia muda,mahitaji na nguvu aliyonayo katika kukamilisha jambo hilo. Kwa tafsiri yangu mtu akiweza kuishi katika hayo anakuwa ameweza kujitawala vizuri.

Katika uongozi wa nchi huu ni utawala wa tano kuwepo tangia Tanzania imepata uhuru,ukianzia kwa mwalimu Nyerere,Mwinyi,Mkapa,Kikwete na hatimaye Rais Magufuli. Katika awamu zote hizo zilizopita watu walihusisha matatizo yao ya kiuchumi na mfumo wa maisha kwa ujumla na utawala uliokuwepo!

Mfano wakati wa Mkapa kuna kipindi umaskini au ukosefu wa pesa uliitwa ukapa,kipindi cha Jakaya Kikwete vivyo hiyvo watu walihusisha umaskini na ukosefu wa pesa na utawala wa Kikwete. Muda huu tukiwa chini ya Rais wa awamu ya tano Dkt JPM, utawala wake bado unalaumiwa kwa kuwa chanzo cha watu kukosa pesa. Natabiri hata utawala wa awamu ya sita hali itakua hivyo hivyo.

Lengo langu sio kukataa kuwa kama serikali na viongozi wake hawana la kulaumiwa katika haya la hasha! Lengo langu ni kusema kumbe inaonekana pengine ndiyo hali halisi ya viongozi wetu kushindwa kukidhi mahitaji yetu tunayodhani wanaweza kututatulia. Kumbe hili ni tatizo sugu kwa Afrika na pengine lisije kuisha mpaka pumzi yako ya mwisho itakapokata! Kwahiyo utaendelea kuishi ukilaumu tawala zote zimepita kuwa ndo sababu ya wewe kutofanikiwa?

Vipi kuhusu utawala wako wewe binafsi? Ni kweli unaishi katika malengo uliojiwekea? Ni kweli matumizi ya rasimali zako unazomiliki unazitumia sawa sawa na inavyotakiwa?

Vipi muda unaotumia katika kufanikisha ndoto na malengo ulojiwekea maishani? Au unasubiri rais na utawala wa awamu ya sita ndo uje kua suluhisho la matatizo yako?

Katika kipindi ambacho wewe unalalamikia utawala kuna wenzio wanaingiza pesa,katika awamu ulizoishi za uongozi kuna wengine wamepata utajiri na huku wakiishi katika tawala hizo hizo unazolalamikia wewe kuwa hazisaidii wananchi kufanikiwa kuishi maisha yaliyo bora.

Amini utawala wako. Ni kichwa chako ukiweza kuishi katika mipango,nidhamu,ubunifu na kufanya kazi kwa bidii hata ikulu kukiwa kuna jiwe utatusua. Wakati tukiendelea kupigania misingi iliyo imara na yenye kumwezesha mwananchi kufanya shughuli zake katika ustawi mzuri kwa maana ya kuhakikisha utawala wa nchi unawanufaisha wananchi lazima uhakikishe utawala wako mwenyewe unafanya kazi kwa kadri na kiwango kinachotakikana.

Post a Comment

 
Top