0

Linah amesema anatamani kuzaa na mwanaume mwenye sifa kama za rapper Darassa.

Muimbaji huyo amesema kwa jinsi ambavyo amewahi kukaa na Darassa na kumsikia akiongea kwa muda mfupi, alibaini kuwa anaweza kuwa baba mzuri.


“Ni mtu ambaye ana sifa zote za kuweza kuwa mwanaume ambaye namtaka. Namchukulia kama kaka yangu yaani sijawahi kumfeel kimapenzi lakini nimekaa naye kwa muda mfupi, nimemuona ni mtu fulani mwenye busara. Ni mwanaume ambaye nikimuona nasema ‘this guy, I wish ningekuwa nina hisia za kimapenzi naye. Katika wasanii wote I wish my boyfriend angekuwa hivi,” Linah ameiambia 255 kwenye kipindi cha XXL cha Clouds FM.


Ameongeza kuwa Darassa anajua kuwa anakumbali na rapper huyo pia anamkubali Linah na ukaribu wao ni wa kama kaka na dada tu.

Post a Comment

 
Top