0

Young Dee amekanusha tena uvumi ulioenea mtaani kuwa anajihusisha na matumizi ya dawa za kulevya.

Akiongea kwenye kipindi cha Harakati cha Clouds FM kinachoendeshwa na Kalapina, rapper huyo amesema tokea akiwa mdogo amekutana na mambo mengi ya kuzushiwa.

“Hata mimi nasikia sana,” alijibu alipoulizwa kuhusu tetesi za kutumia unga. “Unajua mimi nimekuwa kwenye muziki tokea niko mdogo maana tokea nipo shule nimekutana na mengi sana. Nina imani mti wenye matunda ndio hupigwa mawe, unajua sometimes wanavyosema ukifuatisha ndio unaweza kukuta kweli unaingia huko. Lakini situmii madawa ya kulevya, mimi ndio najua maisha yangu, mimi najua natumia pombe tu,” alisema Young Dee.

Alipoulizwa kwanini aliamua kuandika ujumbe kuhusu Babutale kumsaidia Chid Benz na kama hakukubaliana na Tale haya ndio yalikuwa majibu yake:

“Mimi nilihisi kitu tofauti kabisa maana Chid ni msanii mkubwa sana na haikutakiwa kumweka vile, ilitakiwa umchukue umweke sawa kimya kimya na sio vile kila mtu aone. Kama unamsaidia huo ndio ulikuwa mtazamo wangu wa tofauti, hayo mambo mengine yaliyotokea na mimi ni binadamu.”

Post a Comment

 
Top