Hakimu mmoja nchini
 Brazili amefunga mawasiliano ya mtandano wa simu kwa njia ya whatsapp 
kwa saa 72.Hakimu huyo Marcel Montalvao amesema kampuni inayomiliki 
mtandao huo imeshindwa kusaidia kutoa taarifa katika kesi ya uhalifu.
Whatsapp mtandao unaomilikiwa na Facebook umesema umekatishwa tamaa na kitendo hicho kwa kuwa wamekuwa wakitoa ushirikiano wa kutosha mahakamani.
Mtandao huo umekuwa ukifungiwa mara kadhaa nchini Brazil kwa miezi michache ya karibuni kwa sababu zinazofanana na hizo.

Post a Comment