0
WengerMeneja wa Arsenal Arsene Wenger amesema alitarajia mashabiki zaidi waonyeshe kutoridhishwa naye wakati wa mechi ya Jumamosi dhidi ya Norwich.
Arsenal walishinda 1-0.

Wenger atatimiza 20 kwenye usukani Arsenal Oktoba mwaka huu lakini mara yake ya mwisho kushinda ligi ilikuwa 2004 na baadhi ya mashabiki waliinua mabako ya kusema “wakati wa mabadiliko umefika” uwanjani Emirates.

"Nilidhani uwanja wote ungegeuka na kuwa wa rangi nyeupe (kutokana na mabango),” amesema.
"Lengo letu kuu ni kuwafanya watu wote 100% wafurahi. Kwa bahati mbaya, hatukuweza kufanya hilo msimu huu.”

Ushindi wa Jumamosi uliwawezesha Arsenal kuwapita Manchester City, ambao watakuwa wenyeji wa The Gunners uwanjani Etihad Jumamosi, na kutua nambari tatu jedwali la Ligi ya Premia
Arsenal wanahitaji alama mbili kutoka kwa mechi zao zilizosalia kujihakikishia nafari katika Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya msimu ujao, kwa mara ya 18 mtawalia.



Arsenal
Wakati wa mechi hiyo ya Norwich, baadhi ya mashabiki walinyanyua mabango dakika za 12 na 78 za mechi, kuachilia miaka 12 tangu Arsenal walipotawazwa mabingwa ligi mara ya mwisho.
Lakini kunao wengine walioeleza uungaji mkono wao kwa Wenger.
"Mimi ni mtu wa soka. Mimi si mwanasiasa,” alisema Wenger, 66.

"Simo katika mfumo wa demkrasia. Nitakuwepo mechi ijayo, kusimamia mechi, kujaribu kufanya vyema na nakubali maoni ya watu,” alisema.

Mkataba wa Wenger utamalizika msimu wa 2016/17 na anasema hapangi kung’atuka kabla ya wakati huo.

Post a Comment

 
Top