Serikali
imewaagiza Maafisa maendeleo ya Jamii na maafisa ustawi wa Jamii wa
wilaya,kata na mikoa nchini kuwafatilia wanaume wanaowapa ujauzito
watoto wa shule na kuwafikisha Mahakamani.
Akizungumza
leo bungeni katika kipindi cha maswali na majibu Waziri wa Afya
Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu, amesema
serikali haitamvumilia mwanaume yoyote anaempa mwanafunzi ujauzito.
Mhe.
Ummy amesema kuwa serikali ya awamu ya tano itawachukulia hatua wanaume
wote na hakutakuwa na huruma juu ya hilo huku akisisitiza wanawake
ambao si wanafunzi ni wengi mitaani.
Hapo
awali Akijibu Swali la Mbunge wa Ileje, Mhe. Janeth Mbene, Naibu Waziri
wa TAMISEMI, Mhe. Seleman Jaffo amesema kuwa tatizo la watoto kupewa
ujauzito nchini linatokana na vishawishi wanavyokutana wakiwa njiani
wakati wanakwenda mashuleni.
Post a Comment