WAKUU
wa nchi za Afrika wametaka kuwepo na juhudi za pamoja katika
kukabiliana na majanga yatokanayo na mabadiliko ya tabiachi
yanayolikumba bara hilo.
Kauli
hiyo ilitolewa jana mchana (Jumanne, Mei 24, 2016) wakati wa
majadiliano baina ya viongozi kutoka Zambia, Chad, Nigeria, Msumbiji na
Tanzania mara baada ya ufunguzi wa Mkutano wa 51 wa Mwaka wa Benki ya
Maendeleo ya Afrika (AfDB) uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano cha
kimataifa wa Mulungushi, jijini Lusaka, Zambia.
Wakishiriki
kwenye mjadala wa Wakuu wa Nchi na Serikali uliohusu Nishati na
Mabadiliko ya Tabianchi, viongozi hao walisema bara la Afrika linahitaji
kupata maendeleo zaidi licha ya tatizo la nishati linalolikumba bara
hilo hivi sasa.
Akichangia
mjadala huo, Rais wa Zambia, Bw. Edgar Lungu alisema nchi yake imepania
kuboresha hali ya upatikanaji wa umeme vijijini lakini imekuwa
ikikabiliwa na tatizo la uhaba wa mvua kwa zaidi ya miaka miwili hali
ambayo alisema imechangia kukosekana kwa umeme katika maeneo mengi
nchini humo.
“Uhaba
wa mvua umepunguza kiwango cha maji katika bwawa la Kariba ambalo
hutumika kuzalisha umeme nchini mwetu. Na hapa kwetu, karibu asilimia 80
ya umeme wetu, unategemea uzalishaji wa umeme kutokana na vyanzo vya
maji,” alisema.
Rais
wa Chad, Bw. Idriss Deby Itno aliitaka benki ya AfDB ichukue nafasi ya
mdau mkuu kwenye uwekezaji wa sekta ya nishati na kuzisadia nchi za bara
hili kupata mitaji ya uwekezaji na ushauri wa kitaalamu.
“Tunahitaji
kutumia fursa ambazo benki yetu inazo katika kukabilianana changamato
za ukosefu wa nishati. Tukiweza kutekeleza jambo hilo, tutafanikiwa kuwa
na miradi ambayo ni makini na kwa maana hiyo tutaweza kuliangaza bara
letu la Afrika kwa kupata mwanga wa uhakika,” alisema.
Kwa
upande wake, Makamiu wa Rais wa Nigeria, Prof, Yemi Osinbajo alisema
bara la Afrika halina budi budi kuweka kipaumbele kwenye masuala ya
maendeleo yake wakati likitafuta suluhisho la kukabiliana na athari za
mazingira.
“Tunapaswa
kutafuta njia za kubalance mahitaji makubwa ya umeme ambayo bara letu
linakabiliwa nayo dhidi ya athari za kimazingira ambazo zinapigiwa
kelele na mataifa makuna na zinahatarisha kutunyima fursa ya kuendelea
haraka kama ilivyokuwa kwao,” alisema na kuongeza:
“Kama
nchi zilizoendelea zinataka sana kupunguza athari zitokanazo na
mabadiliko ya tabianchi, zinatakiwa zitupatie fedha, teknolojia na
wataalamu ambao watasaidia kuendesha mitambo ili tupate nishati safi
kutokana na mafuta ya petroli na dizeli sababu ni rasilmali ambazo
tunazo.”
Waziri
Mkuu Kassim Majaliwa alisema ili kuondokana na tatizo la nishati, kuna
haja ya kuwa na viongozi wenye utashi wa kisiasa ambao watakuwa tayari
kuruhusu uwekezaji mkubwa kwenye sekta ya nishati na kuongeza kuwa
Tanzania inapitia upya sheria zake ili kuruhusu miradi mikubwa ya
uwekezaji kwenye sekta hiyo.
Aliwaambia
washiriki wa mkutano huo kwamba milango ya uwekezaji Tanzania iko wazi
kwa ajili ya wawekezaji walio tayari kuwekeza kwenye sekta hiyo na
kutaja fursa ambazo Tanzania inazo kwenye sekta ya nishati ikiwemo gesi
asilia, makaa ya mawe, madini ya urani, maji, upepo na nishati ya joto
kutoka ardhini (geothermal energy).
Naye
Waziri Mkuu wa Msumbiji, Bw. Carlos Agostinho do Rosário alisema kuna
haja ya kuwa na taasisi ya uzalishaji na ugawaji umeme ya pamoja
(electricity pool) ambayo itaruhusu wazalishaji wa umeme wawauzie
wanunuzi wakubwa.
Waziri
Mkuu ambaye yuko Lusaka kuhudhuria mkutano huo wa ADB kwa niaba ya
Mheshimiwa Rais, Dk. John Pombe Magufuli, amerejea nchini leo (Jumatano,
Mei 25, 2016).
Post a Comment