Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemteua
Waziri Mkuu Mstaafu Mheshimiwa Mizengo Peter Pinda kuwa Mkuu wa Chuo
Kikuu Huria cha Tanzania (OUT).
Mheshimiwa
Mizengo Peter Pinda anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Balozi Dkt.
Asha-Rose Mtengeti Migiro ambaye ameteuliwa kuwa Balozi wa Tanzania
nchini Uingereza.
Taarifa
iliyotolewa leo tarehe 25 Mei, 2016 na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John
Kijazi imeeleza kuwa uteuzi wa Mheshimiwa Pinda unaanza mara moja.
Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es salaam
Post a Comment