0


Salah Abdesalam, ambaye ndiye mshukiwa mkuu wa shambulizi la kigaidi liliyofanyika mjini Paris, Ufaransa, anatarajiwa kuhojiwa hii leo Ijumaa na wachunguzi wa Ufaransa, kwa mara ya kwanza tangu alipohamishwa kutoka Ubelgiji mwezi uliopita.

Ushahidi wake unatarajiwa kutoa mwangaza kuhusu mipango na mikakati iliyotumiwa na wanamgambo wa Kiislamu katika kutekeleza shambulizi hilo.

Huenda pia akaelezea kuhusu uhusiano uliopo kati ya mashambulizi ya Paris na yale ya Brussels, Ubelgiji, hasa kwa sababu yote mawili yalitekelezwa na kundi moja – la Islamic State.

Abdesalam aliashiria kutohusika sana katika mashambulizi hayo wakati wa mahojiano aliyofanyiwa awali, huku akisema kwamba alitumiwa tu katika mpango uliobuniwa na mtu aitwaye Abdelhamid Abaaoud.

Post a Comment

 
Top