Mchezaji wa kikapu Marekani (NBA) Steven Adams wa timu ya Okhlohamio City ameomba radhi baada ya kuwaita ‘nyani wadogo’ wachezaji wa timu pinzani ya Golden State Warriors waliowafunga bao 108-102. Adams aliyasema maneno hayo baada ya kuhojiwa mwisho wa mchezo.
Adams bado alikuwa akiendelea kudai kuwa hakumaanisha chochote kibaya bali ametumia kama usemi tu akisema “lilikua
ni neno tu nimetumia kama maneno mengine, sikujua kama litamuudhi wala
kumkera mtu yeyote,ila ninaomba radhi lilikuwa tu kama neno nikielezea
jinsi gani wale jamaa walikua na mbio sana”
Post a Comment