Akili nyingi ni zawadi na laana. Wanapojiangalia kwenye kioo, wanawake
wenye akili nyingi huona picha ya mtu mwenye nguvu mwenye malengo,
anayejua anachotaka. Kuwa na akili nyingi ni kitu muhimu kuwa nacho,
lakini wakati mwingine kinaweza kuwatisha wengine.
Pengine ndio maana watu wenye akili nyingi hupata shida ya kupata pendo.
Kama unajiuliza kwanini bado upo single, hizi ni sababu tano kwanini
unaweza ukawa unapata shida kupendwa.
1. Unakuwa mchambuzi mno
Wasichana wenye akili mara nyingi huchambua sana vitu. Huwa na shaka na
kesho yao, njia nzuri za kuimarisha mahaba, na wanataka sana kumpata mtu
sahihi. Hiki hata hivyo sio kitu kibaya.
2. Unajua ni bora kuwa peke yako kuliko kuwa na mwenza asiye sahihi
Na hakuna tatizo katika hilo pia. Watu wenye akili wako makini katika
kumpata mwenza sahihi ambapo wanaweza kuamua kubaki wenyewe kama
asipopatikana.
3. Unajua kuwa mahusiano mara nyingi hufa
Hawa hujua ukweli unaouma kuwa mahusiano mengi hayafiki popote. Matokeo
yake, wakati mwingine hufanya mambo pole pole na kuwa na shida katika
kuingia miguu miwili. Lakini mwenza sahihi ataelewa hilo.
4. Unaweza kuwa unaogopesha
Sio kwamba watu wenye akili huwatisha mambumbu lakini hata wenye akili
pia. Wanaweza wasiwe comfortable na ukweli kuwa unafanya vizuri katika
eneo la maisha ambayo hawapo.
5. Unajua kujilinda mwenyewe
Watu wenye akili katika dunia hii wanaelewa sana hatari katika hali
yoyote na hiyo inahusisha pia dating. Huwa makini, waangalifu na huweka
vikwazo kujilinda wenyewe.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

Post a Comment