0


Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita ameshauri kufungwa kwa kamera maalumu  za CCTV kwenye  nyumba zote za kulala wageni na hoteli ili kuimarisha ulinzi.

Ushauri huo wa Mwita unakuja baada ya  siku sita  kupita , kutokea kwa tukio la mwanamke mmoja kufariki dunia akiwa gesti.

Mwita ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Vijibweni (Chadema), alisema mamlaka husika wakiwamo wamiliki wa hoteli na nyumba hizo waliangalie suala hilo kwa jicho la tatu kwani litasaidia kwa kiasi kikubwa kuzuia matukio kama hayo.

“Kamera hizi zisifungwe chumbani bali zifungwe maeneo ya nje  na mapokezi kwenye jingo husika.Hii ni njia sahihi ya kupambana na matukio kama haya maana hili lipo hivi linaweza kutoke lingine zaidi ya hili,” alisema Mwita ambaye alishika madaraka hayo Machi 22mwaka huu.

Mbali na hilo, Mwita alisahauri pia kuboreshwa kwa mfumo usalama katika maeneo mbalimbali ili kuzuia vitendo kama hivyo vya kinyama vinavyokatisha uhai wa binadamu.

Hata hivyo , Mwita  aliwaomba viongozi wa dini wa mkoa wa Dar es Salaam, kuendelea kutoa elimu kwa umma ili wakazi wa jiji hilo kumrudia Mungu na kuachana na vitendo vya kinyama.

Pia meya huyo amekanusha taarifa zilizosambazwa kwenye  mitandao ya kijamii zikimnukuu yeye kuwa ameshauri wamiliki wa gesti  kuwapiga picha wageni wanaokwenda kulala kwenye nyumba hizo.

Hivi karibuni mwanamke huyo jina limehifadhiwa alikutwa amefariki dunia kwenye gesti  Bray iliyopoa maeneo Kimara , manispaa ya Kinondoni huku chanzo cha kifo bado hakijawekwa wazi hadi uchunguzi utakapokamilika na maiti huyo amehifadhiwa Hospitali ya Mwananyamala.

Post a Comment

 
Top