Katibu
Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Uchukuzi) Mhandisi
Dkt. Leornad Chamuriho ameupa siku mbili uongozi wa Bandari unaosimamia
Mita ya Kupimia mafuta nchini (Flow Meter) iliyoko Kigamboni jijini Dar
es salaam kuhakikisha kuwa unatoa taarifa ndani ya siku mbili kuhusu
hitilafu iliyojitokeza kwenye mfumo wa kufungua valvu za mita hiyo
upande wa umeme.
Aidha,
ameuagiza uongozi huo kutoa taarifa kuhusu hitilafu ya kamera 2 za
usalama zilizoungua na kushindwa kufanya kazi kwa takribani mwezi mzima.
Katibu
Mkuu huyo ametoa maagizo hayo mara baada ya kufanya ziara ya kushtukiza
katika mita hiyo eneo la mji Mwema Kigamboni leo jijini Dar es salaam
na kubaini upungufu wa utendaji wa baadhi ya maeneo.
Maeneo
hayo ni pamoja na kamera za kufuatilia mwenendo wa usalama wa mita
hiyo, valvu zilizoshindwa kufanya kazi upande wa mfumo wa umeme hivyo
kubakiwa na njia ya analoji kutokana na hali ya mvua zilizokuwa
zikiendelea kunyesha jijini Dar es salaam.
“Ifikapo
Jumatatu nipatiwe taarifa kuhusu matengenezo ya vifaa hivi, hatua
zilizochukuliwa na mnieleze lini ukarabati wake utakamilika pia ujenzi
wa paa kuzuia athari ya mvua kwenye mita hii” amesema Dkt. Chamuriho.
Ameongeza
kuwa dhumuni la Serikali ni kuhakikisha vifaa hivyo vinafanya kazi
katika viwango vinavyostahili ili kulinda mapato yanayotokana na mafuta
yanayoingia nchini ili Serikali ipate kodi halali na hivyo kuongeza
mapato ya nchi na kuondoa malalamiko kwa wateja.
Kwa
upande wake Meneja Mradi wa Ujenzi wa Mita hiyo kutoka Mamlaka ya
Bandari nchini Mhandisi Mary Mhayaya ameeleza kuwa uharibifu wa vifaa
hivyo umesababishwa na mvua zilizonyesha hivi karibuni na tayari vifaa
hivyo vimeanza kukabarati.
"
Kisichofanya kazi ni mfumo wa kufungua mafuta upande wa umeme kwenye
baadhi ya valve, upande wa analoji unafanya kazi vizuri na kazi ya
upakuaji mafuta kupitia mfumo wa analojia inaendelea kama kawaida" Amesisitiza.
Amesema kuwa tayari wamemweleza mkandarasi aliyefunga vifaa hivyo kuvifanyia marekebisho haraka iwezekanavyo.
Naye
Kaimu Meneja wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) Hebel Mhanga amesema
kuwa ofisi yake inajukumu la kuhakikisha inatoa huduma sahihi kwa wateja
wanaotumia mitambo hiyo iliyopo bandarini hapo na Serikali inapata
mapato kulingana na huduma iliyotolewa.
Mita
ya Kupimia Mafuta yalnayoingia nchini iko katika hatua ya majaribio kwa
kipindi cha mwaka mmoja ambapo tayari meli tatu zimefanyiwa majaribio
ya upakuaji wa mafuta huku moja ikiwa imefanyiwa vipimo.
Post a Comment