Watu wasiofahamika wamechoma moto Kanisa Katoliki Kigango cha Nyarwele, Parokia ya Kimiza, Jimbo la Kayanga wilayani Karagwe, Mkoa wa Kagera.
Katika tukio hilo la jana usiku, mali zote zilizokuwamo ndani ambazo thamani yake haijajulikana ziliteketea.
Shuhuda
wa tukio hilo, Paulina Nkuba (67) alisema alifika eneo la tukio asubuhi
baada ya kupewa taarifa na mjukuu wake anayesoma Shule ya Msingi
Kimiza.
Alisema baada ya kufika katika eneo la tukio alipiga
yowe kuomba msaada na alipoona watu hawatokei, alitoa taarifa kwa
uongozi wa kitongoji ndipo waliwajulisha wananchi na kuanza kukusanyika.
Paroko wa Parokia ya Kimiza, Padre Fortunatus Bijura alisema kitendo hicho ni cha kuhuzunisha na kusisitiza hawataacha kusali kwa kuwa hata chini ya mti watafanya ibada.
Paroko wa Parokia ya Kimiza, Padre Fortunatus Bijura alisema kitendo hicho ni cha kuhuzunisha na kusisitiza hawataacha kusali kwa kuwa hata chini ya mti watafanya ibada.
Askofu wa jimbo hilo, Almachius
Vicent Rweyongeza aliwataka waumini wasilipize kisasi hata kama wakimjua
aliyechoma kanisa hilo.
Mwenyekiti wa kamati ya kanisa hilo,
Sabas Kafuba alivitaja baadhi ya vitu vilivyoteketea kuwa ni jengo,
nyaraka, meza, viti, kinanda na jenereta.
Akizungumza na
wananchi, ofisa upelelezi wa Wilaya ya Karagwe aliyejitambulisha kwa
jina la Masoud aliwataka kuunda vikundi vya ulinzi na kutoa taarifa za
kukomesha uhalifu huo.
Post a Comment