1.Wapinzani wa Donald Trump wamejitoa wote baada ya matumaini yao kumzuia kushindikana.
2.Hakuna namna tena ya kumzuia billionea Donald Trump kuwa mgombea urais wa Republican.
3.Chama cha Republican kinashuhudia mgawanyiko na mpasuko mkuwa kabisa kuwahi kutokea kuliko wakati mwingine wowote.
3.Wanachama wa Republican wameonekana kuchoma moto kadi zao za uachama kama hasra zao kwa mgombea ambaye hawamtaki.
4.Wapo wanaosema hawatashiriki kabisa kupiga kura uchaguzi mkuu kwa kuwa
Donald Trump hawamtaki na hawawezi kumpigia kura Hillary Clinton.Wapo
ambao wanajiondoa katika chama.
5.Wapo wanaosema watalazimika kumchagua Hillary Clinton maana hawako tayari kuona Donald Trump anakuwa Rais wa Marekani.
6.Wapo wanaoona ni bora tu wakubaliane na hali na kumuunga mkono mtu ambaye hawamtaki kwa manufaa ya chama.
7.Aliyekuwa Rais wa 41 wa Marekani George H.W Bush mwenye umri wa miaka
91 amesema atajiweka kando katika uchaguzi huu na hana mpango wa
kumuunga mkono Donald Trump.
hii ni mara ya kwanza kwa George H.W Bush kutomuunga mkono mgombea wa chama chake cha Republican katika chaguzi zote.
8.Aliyekuwa rais wa 43 wa Marekani George W Bush(Junior ) naye amesema
atajiweka kando katika uchaguzi huu na hatamuunga mkono Donald Trump.
NB:Marais wastaafu wa Republican walio hai ni hawa Bush wawili kwa maana ya baba na mwana.
9.Aliyekuwa mgombea Urais wa Republican 2012 Mitty Romney amesema
hatamuunga mkono Donald Trump na ameenda mbali zaidi kwa kusema kuwa
hata kwenye mkutano mkuu wa kumtanganza mgombea pale Cleveland
hatashiriki.
10.Aliyekuwa mgombea Urais wa Republican 2008 John McCain naye yupo
mbioni kutoa taarifa rasmi.Taarifa za awali zinadokeza kuwa naye
atachukua msimamo wa kutomuunga mkono Donald Trump na atajiweka kando
katika uchaguzi huu.
11.Matajiri wapenzi wa chama nao wamegawanyika kama ilivyo hapo juu kwa
makundi mengine wapo ambao wameonekana tayari kumuunga mkono Hillary
Clinton kwa kuandika hadharani kauli mbiu ya Hillary Clinton I AM WITH
HER (wakimaanisha wanamuunga mkono Hillary Clinton na si mgombea wa
chama chao).
Joseph Mshinga.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment