Jumuiya
ya Vijana CUF (JUVICUF) imeitaka Serikali kubeba mzigo wa kushindwa
kuwajibika ipasavyo kwa kuruhusu uingizwaji wa simu feki nchini.
Kauli ya jumuiya hiyo imekuja wakati imebaki mwezi mmoja kwa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), kuzima simu feki zote.
Akizungumza
na wanahabari jijini Dar es Salaam jana, Katibu Mtendaji wa JUVICUF,
Mahamoud Mahinda Ally alisema Serikali ilishindwa kutimiza wajibu wake
wa kuhakikisha simu hizo haziingizwi nchini, hivyo inapaswa kuwajibika.
Ally alisema Serikali ilipaswa kuziba mianya hiyo tangu mwanzo na kwamba inachofanya sasa ni kukosa huruma kwa watu wake.
Alisema
kitendo cha wananchi kuachwa wakinunua simu feki siku za nyuma bila ya
kudhibiti uingizwaji wake nchini ni kutozingatia matakwa ya haki za
binadamu.
“Kuruhusu simu feki ziingie nchini, kisha kuzizima ni mapambano ambayo Serikali inapambana dhidi ya wananchi wake,” alisema Ally.
Akizungumzia
kuhusu hilo, Meneja Mawasiliano wa TCRA, Innocent Mungy alisema mamlaka
hiyo ilianza kutoa elimu kuhusu ya matumizi ya simu feki tangu mwaka
2010.
Alisema
bado TCRA inaendelea na kampeni hiyo kwa wananchi juu ya madhara ya
matumizi ya simu feki. Pia, alisema TCRA iliamua kufanya hivyo kutokana
na majangili wanaotumia njia za panya kupitisha simu hizo na bila kulipa
kodi.
Alisema
wafanyabishara hao wasio waaminifu ndiyo wamechangia kuwapo kwa
uingizaji wa simu feki nchini, licha ya Serikali kupiga marufuku.
Mungy
alisema kutokana na wimbi la uingizwaji wa simu feki kuwa kubwa,
waliamua kutumia teknolojia ya kuzima simu feki, ambayo itatumika
kuanzia mwezi ujao ili kuwaepusha wananchi na bidhaa hizo kama
zinazofanya nchi mbalimbali duniani.
Katibu
Mtendaji wa Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Mawasiliano
Tanzania (TCRA-CCC), Mary Msuya alisema simu feki kuingizwa nchini ni
tatizo la wafanyabiashara wasio waaminifu.
Alisema
kuna baadhi ya wafanyabiashara wanaotumia njia za panya kuingiza bidhaa
feki nchini. “Siyo simu tu hata bidhaa nyingine.”
Alisema
ofisi yake ambayo ni washauri wa watumiaji wa huduma za mawasiliano
nchini, imekuwa ikitoa elimu kwa wananchi kuhusu simu feki.
Alisema
wananchi wamekuwa wishauriwa kuhakikisha kuwa wananunua simu katika
maduka ya simu na wahakikishe wanapewa risiti ya dhamana ya muda wa
matumizi ya bidhaa usiopungua miezi 12.
“Mteja asiponunua bidhaa feki hata mfanyabaishara atakosa soko,” alisema.Aliwataka wananchi kuzingatia mafunzo wanayopewa.
Post a Comment