0

         Profesa wa Uchumi ashukiwa kuwa gaidi kwa kufanya hisabati 
 
Profesa wa uchumi kutoka Italia, ameelezea hasira za kucheleweshwa katika angatua ya Philadelphia Marekani kwa sababu eti mmoja wa abiria aliyekuwa ameketi karibu yake alimshuku kuwa gaidi kwa sababu alikuwa akifanya hisabati.

Profesa Guido Menzio anasema kuwa alicheleweshwa kuabiri ndege aliyokuwa amepanga kusafiri nayo akihojiwa na maafisa wa usalama wa uwanja huo wa ndege.

Yamkini mwanamke mmoja alikuwa amewanong'onezea maafisa hao kuwepo kwa tishio la usalama kutokana na hisabati ya Profesa huyo.

Profesa Menzio, mwenye nywele nyeusi na rangi ya hudhurungi alikuwa ameratibiwa kupanda ndege iliyokuwa ikitokea Philadelphia, Marekani.
  Profesa wa Uchumi ashukiwa kuwa gaidi kwa kufanya hisabati
Profesa Guido Menzio anasema kuwa alicheleweshwa kuabiri ndege aliyokuwa amepanga kusafiri nayo akihojiwa na maafisa wa usalama
Mwanamke huyo kwa mujibu wa Profesa Menzio alionekana kuwa na hofu.
Kisirisiri mwanamke huyo alipitisha ujumbe kwa mhudumu mmoja wa ndani ya ndege alipomuona profesa akifanya hesabu, alimfikiria kuwa ni gaidi..

Professor Menzio tena alihojiwa kwa urefu na rubani na afisa mmoja.
Baadaye alisema, itifaki ya usalama ya shirika hilo la ndege ni ngumu sana , na inategemea abiria ambao pengine ni wajinga.

Post a Comment

 
Top