MKAZI
wa Kijiji cha Mapinduzi Kata ya Kigwe Wilaya ya Bahi mkoani Dodoma
Julietha Sokoine (24) amejifungua watoto wa watatu na ameiomba serikali,
taasisi,mashirika na watu binafsi kumpatia msaada wa kifedha
utakaomsaidia kuwatunza watoto hao.
Pia alisema msaada huo pia utamuwezesha kupata tiba ya ugonjwa wa pumu ambao umemsababisha kuvimba mwili wote.
Akizungumza
mwishoni mwa wiki, Sokoine ameiomba jamii kumsaidia kutokana na
kukabiliwa na tatizo la ugonjwa wa pumu ambao pia umesababisha kuwa na
hali ngumu ya kimaisha ambayo inamfanya kushindwa kuwatunza vizuri
watoto wake.
Alisema
watoto hao, Daniel Sokoine,David Sokoine na Davis Sokoine walizaliwa
kwa pamoja Machi 22, mwaka huu katika hospitali ya mkoa wa Dodoma huku
kati ya wawili wa wakiwa na uzito kilo mbili na nusu na wa mwisho kilo
mbili.
“Hali
yangu siyo mzuri kutokana na mimi mwenyewe kukabiliwa na tatizo la
ugonjwa wa pumu,ambapo wakati mwingine nalazimika kuwanywesha maziwa ya
ngombe watoto hao pindi ninapozidiwa na ugonjwa huo”alisema .
Kwa upande wake baba wa watoto hao Sokoine Chipanta alisema pamoja na juhudi za kilimo hata hivyo mazao yake yalinyauka na jua.
Alisema
kutokana na hali hiyo analazimika kutafuta vibarua ili kuweza kupata
fedha kwa ajili ya kununua chakula pamoja na matunzo ya watoto hao.
Alisema kwa wale wote watakaoguswa na kuamua kumpa msaada wawasiliane naye kwa namba ya simu +255 652 744 510.
Post a Comment