WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye, amenunua nakala moja ya albamu ya Injili ya msanii na prodyuza, Goodluck Gozbert, kwa Sh milioni 3 kutokana na kuguswa na ujumbe uliopo katika albamu hiyo.
Waziri huyo alinunua albamu hiyo wakati wa uzinduzi wa albamu hiyo ya kwanza ya msanii huyo iliyopewa jina la ‘Ipo Siku’ uliofanyika Mwanza.
“Albamu yangu ilimgusa sana Waziri Nape Nnauye na yeye kwa kuniunga mkono amenunua nakala moja ya albamu kwa shilingi milioni 3 na kuamsha ari kwa vingozi wengine waliohudhuria uzinduzi huo,” alieleza Goodluck.
Albamu hiyo inabebwa na nyimbo ‘Acha Waambiane’, ‘Hao Hao’, ‘Nimesamehe’, ‘Ndiwe Mungu’, ‘Pendo Langu’, ‘Moyo Tulia’, ‘Surprise’ na ‘Ipo Siku’ iliyobeba jina la albamu.
Post a Comment