Duru za habari zimeripoti kuibuka tofauti kubwa baina ya nchi mbili vamizi za Saudia na Imarat kuhusiana na kadhia ya Yemen.
Mtandao wa habari wa Sa'at Imarat umefichua tofauti hizo kali baina
ya watawala wa Aal Saud na Imarat kuhusiana na kadhia ya Yemen. Tofauti
hizo zimejiri baada ya Abd Rabbuh Mansur Hadi, rais wa zamani wa Yemen
aliyejiuzulu wadhifa wake na kukimbilia Saudia kukosoa misimamo ya
Imarat ya kumpa hifadhi Khaled Bahah, waziri mkuu wa Yemen aliyekimbia
nchi yake. Mansur Hadi,
amekitaja kitendo cha Imarat cha kumpatia hifadhi Bahah kuwa ni kutojali maslahi ya Wayemen na kushadidisha tofauti nchini humo. Itakumbukwa kuwa, mwanzoni mwa mwezi huu, Mansur Hadi alimuuzulu Khaled Bahah wadhifa wake wa uwaziri mkuu na kumpa nafasi hiyo Jenerali al-Ahmar, suala ambalo liliifanya Imarat kuondoa sehemu kubwa ya askari wake vamizi na zana za kijeshi
kutoka nchini Yemen. Mbali na hayo, mashambulizi ya pande mbili dhidi ya maeneo ya kusini mwa Yemen ukiwemo mkoa wa Aden, yamezidisha tofauti za nchi hizo vamizi. Inaelezwa kuwa, safari ya hivi karibuni ya Mohammad Bin Salman Al Saud, mrithi wa kiti cha ufalme nchini Saudia huko Imarat, imefanyika kwa lengo la kujaribu kupunguza tofauti hizo. Itakumbukwa kuwa, tangu
mwanzoni mwa mwaka jana, Saudia kwa kushirikiana na nchi kadhaa za Kiarabu ikiwemo Imarat, ziliaanzisha mashambulizi ya kivamizi nchini Yemen kwa lengo la kutaka kumrejesha madarakani Abd Rabbuh Mansur Hadi, rais wa nchi hiyo aliyekuwa tayari ametangaza kujiuzulu wadhifa huo, njama ambazo licha ya kusababisha mauaji ya maelfu ya watu, zimeshindwa kufikia malengo yake.

Post a Comment