0


Wagabon wapatwa na wasiwasi wa kuibuka machafuko ya kisiasa nchini mwao 
 
Muungano wa kiraia nchini Gabon umeelezea wasiwasi uliowakumba wananchi kuhusu uwezekano wa kutokea machafuko ya baada ya uchaguzi mkuu nchini humo. 
 
Ripoti iliyotolewa na muungano huo wa Guy Réné Mambo Lemboumba imesema kuwa, anga ya wasiwasi na mashaka imetawala nchini humo ikiwa imesalia miezi minne kabla ya kufanyika

uchaguzi mkuu nchini. Ripoti hiyo imeongeza kuwa, Wagabon wengi wanaamini juu ya uwezekano wa kutokea mchafuko kutokana na anga ya kisiasa inayotawala nchini humo hivi sasa na kwamba suala hilo limewafanya kuwa na wasiwasi mkubwa.

Kufuatia hali hiyo, muungano huo umeazimia kuwasilisha ripoti ya malalamiko yake katika ofisi za Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika kuhusiana na kadhia hiyo.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, mapigano na migogoro imeongezeka kuelekea uchaguzi huo. Vilevile taasisi hiyo isiyo ya serikali imetaka kuchukuliwe hatua za kuimarisha usalama na amani nchini Gabon katika kipindi cha miezi minne iliyosalia kabla ya kufanyika uchaguzi mkuu.

Post a Comment

 
Top