0

Zaidi ya watu 77 wamefariki katika tetemeko la kubwa ardhi kuwahi kukumbwa Ecuador katika kipindi cha zaidi ya mwongo mmoja .

Idadi ya waliojeruhiwa ni zaidi ya watu 600.
 
Makamu wa rais wa nchi hiyo ametangaza hali ya tahadhari katika mikoa sita nchini humo, huku maafisa wa huduma za dharura wamepelekwa kusaidia .

Maafisa katika kituo cha Marekani cha utafiti wa kijiologia wamesema tetemeko hilo la ardhi lilikuwa la kiwango cha 7.8 kwenye vipimo vya Richter.
Kitovu chake kilikuwa takriban kilomita 27 kutoka kwa mji wa pwani uitwao Muisne mji ambao kwa kawaida hauna wakaazi wengi.

Taarifa katika mitandao ya kijamii nchini humo zaelezea jinsi mapaa ya majengo na hata baadhi ya madaraja na vivukio vya watembea miguu vilivyoporomoka kutokana na tetemeko hilo.



Stephan Kuffner mwandishi habari anayeishi katika mji mkuu wa nchi hiyo Quito maili 200 kutoka eneo la tukio ameelezea jinsi watu walivyokimbilia kutoka nje ya majengo wakati ardhi ilipanza kutingisika..

Awali Kituo cha kutoa onyo la uwezeano wa kutokea mafuriko, Pacific Tsunami Warning Centre kimesema huenda kukawa na mawimbi makali yatakayoweza kufikia maeneo yaliyokilomita 300 kutoka mahali tetemeko hilo lilipotokea.

Post a Comment

 
Top