Mwanzilishi wa
kampuni ya Tesla Bw Elon Musk amesema kampuni hiyo imepokea oda 276,000
za magari yake mapya Model 3 ambayo yanatumia umeme badala ya mafuta.
Bw Musk, ambaye ndiye afisa mkuu mtendaji wa kampuni hiyo, alisema walipata oda hizo kufikia mwisho wa Jumamosi.
Magari ya kwanza yatawasilishwa kwa wanunuzi mwishoni mwa 2017.
Si wote waliowasilisha oda wanaotarajiwa mwishowe kununua magari hayo.
Wanunuzi wanatakiwa kuweka rubuni ya $1,000 ili kuhifadhiwa magari yao.
Wengi wa waliowasilisha oda wanatoka Uingereza, Jamhuri ya Ireland, Brazil, India, China na New Zealand.
Post a Comment