0

12479390_1264053230275845_15732377_n
Diamond Platnumz ni bingwa wa kuandika nyimbo za kuachwa, kuumizwa na kutendwa kimapenzi.
12479390_1264053230275845_15732377_n
Kamwambie, Mbagala, Mawazo, Ukimwona, Nataka Kulewa, Bado na zingine, zilihit kwasababu ziligusa maisha ya wanaume wengine wahanga wa malavidavi. Lakini staa huyo ambaye hivi

karibuni alisema Zari ameutunza moyo wake kwenye friji kiasi cha masuala ya kuumizwa kuyasikia tu kwa wengine kwa sasa, humkumbuka msichana mmoja kila anapotaka kuandika nyimbo za aina hiyo.
Si Wema wale ex wake mwingine unayemfahamu, Harmonize amemtaja baada ya mimi kumuuliza tetesi kuwa mashairi ya bosi wake huyo kwenye Bado, yalimlenga ex wake, Wema Sepetu.
“Diamond hajaanza kuimba leo mambo ya kuachwa, aliimba Kamwambie, akaimba Mbagala,” Harmonize amesema kwenye Chill na Sky.
“Mimi naamini kabisa, hata mimi mwenyewe nilivyomuuliza ‘kwani ulimuimbia nani Kamwambie?’ akasema mimi nikitaka kuandika nyimbo yoyote ya mapenzi namkumbuka Sarah mwanamke ambaye nilimpenda sana.”
Sikiliza Chill na Sky na Harmonize hapo chini.
Jiunge na Bongo5.com sasa Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo5! Bongo5

Post a Comment

 
Top