0


                                                                    Getty
Mahakama kuu nchini India imewatia hatiani na kuwahukumu kifungo cha maisha maofisa wa polisi wapatao arobaini na saba baada ya kubainika kuwa walihusika katika mauaji ya mahujaji kumi wa jamii ya Sikh yapata miaka ishirini na mitano iliyopita na baadaye maofisa hao kudanganya katika utetezi juu ya shambulio hilo.

Inaarifiwa kutoka upande wa ushahidi kwamba, maofisa hao wa polisi, walilisimamisha basi lililokuwa limebeba familia ya sikh katika jimbo la Uttar Pradesh lililoko upande wa kaskazini mwa India, na kuwalazimisha wanaume kumi kutii amri ya kushuka kwenye basi hilo na kufuatana nao kwenye msitu mnene uliokuwa jirani na kisha wakawapiga risasi wanaume hao.

Baada ya hapo, maofisa hao wa polisi wakatoa utetezi wakadai kwamba wanaume hao walikuwa wanajeshi. Wakati huo,kikundi cha jamii ya Sikh kilichokuwa na silaha kimekuwa kikidai wapewe ardhi yao binafsi ili wajitenge na India kufuatia tukio hilo.

waendesha mashitaka wamedai kwamba maofisa hao wa polisi walifanya shambulio hilo kwa matarajio ya kuja kupongezwa kwa kuwaua wahalifu. Na imefahamika kuwa maofisa wengine kumi waliohusika katika tukio hilo walikwisha fariki dunia.

Post a Comment

 
Top