Rais wa Sudan Omar
al Bashir amesema ataachia madaraka ya nchi hiyo mwaka 2020 ambapo
atakuwa ameongoza taifa hilo kwa jumla ya miaka 30.
Kiongozi huyo anasakwa na mahakama ya kimataifa ya uhalifu ICC kuhusiana na mashtaka ya uhalifu wa kivita na mauaji ya halaki na ukatili dhidi ya binadam ambapo umoja wa mataifa unasema watu milioni mbili na nusu wameyakimbia makazi yao katika mji wa Darful tangu mwaka 2003.
Hata hivyo Al Bashir amekanusha madai ya hivi karibuni ya tuhuma dhidi ya vikosi vya serikali kushiriki katika machafuko ya eneo la Jebel Marra huko Darful.
Post a Comment