Safari ya ndege
iliyokuwa ikitokea uwanja wa ndege wa Manchester ilikatizwa ilikuruhusu
babu mmoja na mkewe kutoa salamu za mwisho kwa mjukuu wao aliyekuwa
akipumua hewa yake ya mwisho hospitalini huko Uingereza.
Habari hizo za kushtua sana ziliponza bibi huyo ambaye alimueleza mhudumu wa ndege hiyo.
Kwa sababu ya huzuni na kububujikwa kwa huruma kutoka kwa abiria wenzake, mhudumu mmoja alikwenda na kumpasha habari hizo rubani wa ndege hiyo ya Etihad.
Kwa mshangao rubani huyo alipunguza kasi ya ndege hiyo na kuomba ruhusa kurejea katika eneo la kuegesha ndege ilikuwapa fursa kushuka na kuelekea hospitalini kumuaga mjukuu wao.
Japo shughuli hiyo ya kuwashusha na kupakua mizigo yao ilisababisha ndege hiyo na abiria wengine kuchelewa, juhudi hiyo ya kipekee ya rubani huyo wa Etihad ilimsababishia kusifiwa na abiria na wapanga safari katika uwanja huo wa ndege.
Post a Comment