Manchester United
wameweka hai matumaini yao ya kumaliza katika nne bora Ligi ya Uingereza
kwa kulaza Aston Villa 1-0 uwanjani Old Trafford.
Matokeo hayo hata hivyo yana maana kwamba Aston Villa wameshushwa daraja.
Villa wanashika mkia wakiwa na alama 16 baada ya kucheza mechi 34.
Newcastle United, walio hatarini ya kushushwa daraja, wamejiwekea matumaini baada ya kulaza Swansea 3-0. Newcastle wana alama 28 kwa sasa.
Matokeo ya mechi zilizochezwa Jumamosi ni kama ifuatavyo:
- Man Utd 1-0 Aston Villa
- West Brom 0-1 Watford
- Newcastle 3-0 Swansea
- Everton 1-1 Southampton
- Norwich City 0-3 Sunderland.
18:55 Mechi zamalizika
- Man Utd 1-0 Aston Villa
- West Brom 0-1 Watford
- Newcastle 3-0 Swansea
- Everton 1-1 Southampton
18:49 Mechi inamalizika: Man Utd 1-0 Aston Villa
Hii ina maana kwamba Aston Villa wameshushwa daraja kutoka Ligi Kuu ya Uingereza.18:46 BAOOOO! Newcastle 3-0 Swansea
Newcastle wanajihakikishia ushindi kwa bao la tatu kupitia Andros Townsend.18:44 West Brom 0-1 Watford
West Brom wanapata penalti ya pili. Lakini kipa Gomes anaokoa tena, mara ya pili.
18:43 Man Utd 1-0 Aston Villa
Rudy Gestede nusura awape Villa bao la kitulizo. Ashley Westwood naye anajaribu lakini hana bahati.
18:39 BAOOOO! Newcastle 2-0 Swansea
Mousa Sissoko anaongezea Newcastle la pili.18: 35 BAOOOO! Everton 1-1 Southampton
Sadio Mane anasawazishia Southamtpon18:34 Man Utd 1-0 Aston Villa
Anthony Martial anaingia nafasi ya mfungaji bao Marcus Rashford zikiwa zimesalia dakika 12 hivi mechi kumalizika.
18:27 BAOOOO! Everton 1-0 Southampton
Ramiro Funes Mori anaweza Everton kifua mbele.18:22 West Brom 0-1 Watford
Wanapata penalti baada ya Berahino kuangushwa. Lakini inaokolewa.
18:22 Man Utd 1-0 Aston Villa
Nahodha Wayne Rooney, ambaye amerudi kucheza juzi baada ya kuuguza jeraha ameondolewa uwanjani. Nafasi yake anaingia Jesse Lingard.
18:22 West Brom 0-1 Watford
West Brom wanaendelea kushambulia Watford.
18:13 Man Utd 1-0 Aston Villa
Memphis Depay anachomoka na kuwachenga wapinzani eneo la hatari na kutoa krosi. Lakini hapati usaidizi.
18:11 West Brom 0-1 Watford
Kipa Heurelho Gomes anawaokoa Watford kutoka kwa mpira wa kichwa wa Gareth McAuley.
18:05 Man Utd 1-0 Aston Villa
United wanaanza kwa kasi. Juan Mata anampata chipukizi Marcus Rashford eneo la hatari. Mkwaju wake hata hivyo unakwepa lango.
18:02 Kipindi cha pili
17:47 Ni wakati wa mapumziko:
- Everton 0-0 Southampton
- Man Utd 1-0 Aston Villa
- Newcastle 1-0 Swansea
- West Brom 0-1 Watford
Villa wanapata nafasi baada ya Jordan Ayew kumchenga Chris Smalling eneo la hatari. Lakini anasita kidogo na Morgan Schneiderlin anamzuia.
17:41 West Brom 0-1 WatfordWest Brom wanajaribu kujikwamua. Saido Berhino anapiga kombora lakini linatoka nje. Stephane Sessegnon naye anajaribu lakini mpira wake unakosa goli pembamba.
17:40 BAOOOOO! Newcastle 1-0 Swansea
Kupitia kona, Jamaal Lascelles anafungia Newcastle.17:39 Everton 0-0 Southampton
Pigo kwa Southampton. Nahodha wao Mreno Jose Fonte anaumia. Mjapani Maya Yoshida anajiandaa kuingia nafasi yake.
17:36 Newcastle 0-0 Swansea
Newcastle wanaendelea kushambulia lakini bahati yao bado haijasimama.
17:31 BAOOOOO! Man Utd 1-0 Aston Villa
Marcus Rashford anawaweka United kifua mbele baada ya kupokea pasi kutoka kwa Antonio Valencia. Sasa amefunga mabao saba katika mechi 12 alizowachezea United.17:31: Man Utd 0-0 Aston Villa
Manchester United wamepata kona tisa kufikia sasa. Lakini hawajaweza kumtatiza kipa wa Aston Villa Brad Guzan
17:27 BAAAOOOO! West Brom 0-1 Watford
Uwanjani Hawthorns, Ben Watson anatikisa wavu.17:26 Newcastle 0-0 Swansea
Gylfi Sigurdsson anateleza akipiga frikiki. Mkwaju wake unapaa juu na kutoka nje.
17:23 Everton 0-0 Southampton
Southampton wameanza kudhibiti mpira. Wamepata naafsi mbili nzuri. Mpira wa Jordie Clasie umepaa juu ya mwamba wa goli. Kombora la Shane Long slashes pia limekosa wavu.
17:18 Man Utd 0-0 Aston Villa
Wayne Rooney anatuma krosi lakini mpira wa kichwa wa Fellaini unatoka nje.
17:15 Everton 0-0 Southampton
Southampton wanashambulia. Mara ya kwanza kupitia Cuco Martina na pili kupitia Mkenya Victor Wanyama. Lakini hawamtatizi kipa mwenyeji Joel Robles.
17:14 Newcastle 0-0 Swansea
Newcastle wanakaribia kufunga. Vurnon Anita anatuma krosi kutoka upande wa kulia lakini kipa wa Swansea anazinduka upesi na kuondoa mpira huo eneo la hatari. Anita anarejea tena na kumwandalia Andros Townsend lakini mpira wa Townsend unatua mikononi mwa Fabianski.
17:13 West Brom 0-0 Watford
Uwanjani Hawthorns, mambo yametulia. Hakuna aliyeona lango la mwenzake.
17:10 Man Utd 0-0 Aston Villa
Leandro Bacuna anatumia kichwa kuwazuia Mata na Memphis kufunga huku United wakiendelea kushambulia.
17:06 Leicester City ambao wanaongoza kwenye jedwali watashuka dimbani kesho dhidi ya West Ham.
17:05 Manchester United wameanza kwa kudhibiti mpira. Mambo bado ni 0-0.
17:00 Wachezaji mechi ya Manchester United na Aston Villa
Man Utd | Aston Villa |
De Gea | Guzan |
A Valencia | Hutton |
Smalling | Clark |
Blind | Lescott |
Rojo | Cissokho |
Fellaini | Bacuna |
Schneiderlin | Westwood |
Mata | Sinclair |
Rooney | Gueye |
Depay | Richardson |
Rashford | J Ayew |
Benchi | Benchi |
Martial | Richards |
Young | Sánchez |
Romero | Gil |
McNair | Bunn |
Lingard | Lyden |
Darmian | Gestede |
Fosu-Mensah | Grealish |
- Everton v Southampton
- Man Utd v Aston Villa
- Newcastle v Swansea
- West Brom v Watford
- Norwich 0-3 Sunderland
- Everton v Southampton 17:00
- Man Utd v Aston Villa 17:00
- Newcastle v Swansea 17:00
- West Brom v Watford 17:00
- Chelsea v Man City 19:30
Post a Comment