WASANII wa filamu za kibongo, Single Mtambalike ‘Richie Richie’ na Elizabeth Michael ‘Lulu’, wameshinda tuzo za Africa Magic Viewers Choice Awards 2016 zilizofanyika juzi katika mji wa Lagos, nchini Nigeria.
Richie alishinda tuzo kupitia filamu yake ya ‘Kitendawili’, akishinda kipengele cha filamu ya Kiswahili, ‘Best Indigenous Language Movie/ TV Series-Swahili’, huku Lulu akishinda kupitia filamu yake ya ‘Mapenzi ya Mungu’ kipengele cha filamu bora Afrika Mashariki, ‘Best Movie- Eastern Africa’.
Washindi wengine ni Frank Raja Arase aliyeshinda mwongozaji bora (Best Art Director Movie/TV Series) kupitia filamu ya ‘The refugees’, Ariyike Oladipo ameshinda (Best Television Series) kupitia filamu ya Daddy’s Girls.
Louiza Calore ameshinda (Best Makeup Artist Movie/TV Series) kupitia filamu ya ‘Ayanda’ ambayo pia imenyakua tuzo ya uandishi bora iliyonyakuliwa na Trish Malone, tuzo ya filamu fupi imenyakuliwa na Oluseyi Amuwa kupitia filamu ya ‘A day with death’.
Post a Comment